Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Friday, June 29, 2018

Baba amuua Mtoto wake kisa Maparachichi

Polisi nchini Kenya linamsaka Mr. Morris Kirema kwa kosa la kumuua Mtoto wake mwenye miaka 12 na kumjeruhi Mtoto wake mwingine mwenye miaka 8 kwa kutumia panga na mateke akiwashutumu Watoto hao kula maparachichi kutoka katika shamba la jirani yao.

Mr. Morris anadaiwa kutumia mateke, ngumi pamoja na panga kuwaadhibu Watoto hao baada ya kula maparachichi kutoka katika shamba la jirani yao na kupelekea Mtoto wake huyo wa kiume mwenye miaka 12 kufa hapohapo.

Kwa upande wa Mtoto wa kike mwenye miaka 8 yeye amejeruhiwa vibaya sana pamoja na Mama yake ambao wanapatiwa matibabu katika hospitali moja nchini humo.

Inadaiwa kuwa mwenye shamba ambalo Watoto hao waliiba maparachichi hayo alidai alipwe kutokana na kitendo walichokifanya Watoto hao na ndipo Mr. Morris alipokasirika na kunuia kuwa lazima atawaua Watoto hao wakirudi kutoka shule.

Aidha duru za kuaminika zinasema kuwa Mwanaume huyo anasumbuliwa na uraibu wa michezo ya bahati nasibu na amekuwa akiwa mchungu akiombwa pesa na Mke wake.
Advertisement
Loading...
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
==

taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )

Loading...