Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Tuesday, June 19, 2018

Basi la SABCO Lapata Ajali na Kuua Mtu Mmoja

Mnamo tarehe 18/06/2018 majira ya saa 13:15hrs mchana katika barabara ya Usagara   – Kigongo Ferry maeneo ya Kingongo Ferry kijiji cha kigongo Ferry kata ya Bukumbi  tarafa ya usagara wilaya ya misungwi mkoa wa mwanza, gari no. T.581 ARL  aina ya scania bus kampuni ya SABCO  iliyokuwa inatokea Mwanza kuelekea Msalala wilaya ya Nyan’gwale mkoa wa Geita likiendeshwa na dereva aliyefahamika kwa jina la Idd Omary miaka 40, Mnyamwezi, mkazi wa Mkuyuni- Mwanza, liiligonga ofisi ya Ferry na kusababisja kifo kwa Zabroni Malando, miaka 37, Msukuma, mfanyabiashara na mkazi wa Sengerema, aliyefariki dunia wakati akipatiwa matibabu katika hospitali ya bukumbi.

 Aidha pia ajali hiyo ilisababisha majeruhi kwa watu kumi (10), wanaume sita (6) na wanawake wa nne (4), wote wapo katika hospitali ya Bukumbi wakiendelea kupatiwa matibabu.

Aidha kati ya hao majeruhi mahututi wapo watatu ambao ni Idd Omary, miaka 40, dereva wa gari lililopata ajali, Ibula  Raphael, miaka 34, msukuma, mkulima na mkazi wa Busolwa na Sophia Lugihila miaka 45, msukuma, mkulima na mkazi wa msalala na wote wamepelekwa hospitali ya Sekouture iliyoko Mwanza kwa matibabu zaidi.

Chanzo cha ajali ni kuferi kwa breki za gari hali iliyopelekea gari hilo kugonga ofisi za ferry na kusababisha kifo na majeruhi. 

Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hospitali ya Bukumbi kwa ajili ya uchunguzi na utambuzi pindi uchunguzi ukikamilika utakabidhiwa kwa ndugu wa marehemu kwa ajili ya mazishi.

Kaimu kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza Kamishina msaidizi wa polisi Mkadamu Khamisi Mkadamu anatoa pole kwa wote hususani kwa  ndugu na jamaa wa marehemu wa ajali hiyo, tunawaombea kwa mwenyezi mungu awape nguvu katika kipindi hiki kigumu. Aidha pia tunawaombea majeruhi wapone haraka ili waweze kuendelea na kazi.

Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )