Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Thursday, June 7, 2018

Bavicha Watoa Kauli kuhusu Kifo cha Maria na Consolata

Baraza la Vijana wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (BAVICHA), limeitaka serikali kujifunza kupitia kifo cha mapacha walioungana, Maria na Consolata ambao wamefariki Jumamosi Usiku wakati wakipatiwa matibabu katika hospitali ya Rufaa Iringa.

Kupitia taarifa ya mwenyekiti BAVICHA, Patrick Ole Sosopi amesema kuwa kama taifa inabidi kukubaliana na ukweli kuwa sekta ya afya ina changamoto nyingi ikiwepo huduma za Afya na uduni wa mazingira hivyo viongozi wanapaswa kushughulikia matatizo hayo na siyo kuwa mbele katika kushiriki misiba.

Amesema kuwa taifa limepoteza nguvu kazi ambao walikuwa na malengo pamoja na ndoto kubwa katika taifa pindi watakapokuwa wamemaliza masomo yao.

Maria na Consolata walizaliwa Novemba 19, 1997 na wamefariki Juni 2, 2018 ambapo enzi za uhai wao walikataa kutenganishwa miili yao na waliishi kwa miaka 21 wakiwa wameungana  hivyo hivyo.

Septemba mwaka jana, baada ya kufaulu mtihani wa kidato cha sita, Maria na Consolata walijiunga na Chuo Kikuu cha Kikatoliki cha Ruaha, Iringa na walianza kuugua maradhi ya moyo na Desemba mwaka jana, wakahamishiwa taasisi ya maradhi ya moyo ya Jakaya Kikwete katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dar es Salaam ambako walilazwa kwa miezi miwili.

Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )