Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Thursday, June 28, 2018

Benki ya Dunia yaikopesha Tanzania Bilioni 780

Benki ya Dunia imeidhinisha mkopo nafuu wa Dola 350 milioni (zaidi ya Sh787.5 bilioni) kwa Serikali ili kuboresha miundombinu ya maji safi na salama.

Taarifa ya benki hiyo iliyotolewa jana , Juni 27 inasema mkopo huo utawanufaisha watu milioni tatu kupata maji safi na wengine milioni nne wakiishi kwenye mazingira safi.

“Jana bodi ya wakurugenzi wa Benki ya Dunia imeidhinisha mkopo huo utakaoinufaisha mikoa 17 kuimarisha upatikanaji wa maji safi na salama vijijini,” inasomeka taarifa hiyo.

Takwimu zinaonyesha watu 11 katika kila 100 hupata maji safi maeneo ya vijijini ambako ni shule moja kati ya kila mbili ina matundu ya vyoo yanayokidhi mahitaji hivyo juhudi za ziada kuhitajika ili kuboresha miundombinu.

Kutokana n ahali hiyo, watoto ndio wahanga wakubwa kwani takwimu zinaonyesha mmoja katika kila watatu hukosa virutubisho muhimu yakiwamo maji ya kutosha.

 Kutokana na mkopo huo, mkurugenzi mkazi wa benki hiyo, Bella Bird anasema kaya 1,250 na shule 1,500 zitanufaika kutokana na jitihada za Serikali kuboresha huduma za umma.

“Ubora wa rasilimaliwatu ni muhimu sana hasa kipindi hiki Tanzania inapojipanga kuelekea uchumi wa kati. Upo uhusiano wa karibu kati ya maji safi na salama na maendeleo ya afya ya mtoto hasa wa kike ambao uhudhuriaji wao shuleni unalegalega nchini,” amesema Bella.
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Loading...
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )