Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Monday, June 18, 2018

Brazil Nayo Yabanwa Mbavu ya Sare 1-1 na Switzerland Kombe la Dunia

Na Magdalena Kashindye
Brazil jana ilishindwa kufurukuta mbele ya Switzerland na kulazimishwa sare ya 1_1 katika mchuano ya kombe la dunia inayoendelea nchini urusi .

Brazil ilikuwa ya kwanza kuliona lango la Switzerland dakika ya 19 ya mchezo kupitia kwa nyota wake aliyeng'aa katika mchezo huu Phillippe Countinho na hadi wanaenda mapumnziko Brazil akiwa kifua mbele.

Kipindi cha pili dakika ya 50 Steven Zubery aliisawazishia timu yake kwa goli Safi la kichwa na hadi mwamuzi anapuliza kipenga cha mwisho Brazil 1_1 Switzerland.

Kwa matokeo  hayo,  Brazil inaongeza idadi ya vigogo wa soka duniani kuanza vibaya .

Kati ya vigogo Sita waliocheza ni Ufaransa pekee ndiye aliyefanikiwa kushinda wakati Ujerumani akipoteza na Argentina, Brazil, Ureno na Hispania zikiambulia sare na kuleta taswira mpya ya ushindani mwaka huu.
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Loading...
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )