Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Tuesday, June 5, 2018

Chemical Afunguka Kuhusu Kutolewa BIKRA Na Vidume Wawili

adv1
Rapa wa kike wa bongo Chemical 'mwana wa Lubao' amefunguka na kudai hawezi kujutia kutokuolewa na mwanaume ambae ametoa usichana wake 'bikra' kwa kuwa anawajua wanaume waliokuwa wengi hawana mapenzi ya kweli huwa wanabadilika muda wowote wakijisikia.

Chemical ametoa kauli hiyo wakati alipokuwa anazungumza kwenye kipindi cha eNewz kutoka EATV na kusisitiza kuwa licha ya kuwa yupo katika mahusiano lakini hana malengo ya aina yeyote kwa kipindi hiki kufunga pingu za maisha 'ndoa' mpaka pale atakapojihakikishia yeye mwenyewe ameweza kukamilisha kila alichokuwa anakihitaji kukipata.

"Sijasema kama ninaingia kwenye ndoa baada ya miaka mitano au 10, 'no' sijasema hivyo. Watu hubadilika sana anaweza mtu akakupenda leo halafu kesho asikupende na kwangu mimi hilo suala nipo fresh kabisa kwa hiyo sijaingia katika mahusiano kwa kusema huyo ndio atakuja kunioa leo wala kesho", amesema Chemical.

Mbali na hilo, Chemical amedai haikuwa jambo rahisi ya yeye kutolewa usichane wake na mwanaume mmoja kwa kuwa alikuwa amekomaa sana hivyo ikapelekea kutembea na wanaume wawili kwa wakati mmoja katika kutekeleza jambo hilo.

"Ujue nimekaa hiyo miaka 20 sio midogo, kwa hiyo ikabidi wasaidiane. Yote hayo yamefanyika nikiwa na akili zangu wala sijatumia pombe maana nilipanga kitolewe na kwa kuwa wa kwanza alishindwa ili bidi aje mwingine amalizie kuitoa", amesisitiza Chemical.
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )