Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Sunday, June 17, 2018

Davido Ampandisha Diamond Kwenye Show Ya Clouds

adv1
Na Amini Nyaungo-Fullshangwe
Muimbaji kutokea Nigeria Davido alifanya show katika Ukumbiwa Next Door Arena ulipo Dar es Salaam ambapo aliambata na wasanii wanao fanya muziki wa bongofleva ambao ni Ruby, Nandy, The Mafik, Aslay na wegine.

Lakini Moja ya Jambo ambalo halikutegemewa na mashabiki ni kumuona msanii Diamond Platnumz akipanda kwenye stage moja na Davido tena waki-perform wimbo wa Number one Remix, wimbo ambao Diamond aliwai kumshiirikisha Davido kipindi cha Nyuma.

Ikumbukwe kuwa Kumekuwa na mgogoro wa chini kwa chini baina ya Diamond na uongozi wa Clouds Media, huku mashabiki wa muziki nchini wakiachwa na sintofahamu. Ngoma za msanii huyo maarufu barani Afrika ni kama zimepigwa marufuku kusikika ndani ya redio ama kuonekana katika televisheni inayomilikiwa na Clouds Media.

Mara kadhaa, msanii huyo amekuwa akisikika akitoa vijembe dhidi ya redio na televisheni hiyo maarufu nchini.

Ukiuliza urafiki wao umeisha vipi hakuna anayejibu sawa sawa, ndio maana Edwini Senzaba amesema mambo ya ‘Ngoswe muachie Ngoswe’.

Mchongo uko hivi, Davido alikuwa na show hapo ambapo imeandaliwa na Uongozi wa Clouds.

Diamond alifanya show huko Dar Live na baada ya kumaliza aliondoka haraka na kwenda Next Door na kuruka na Davido kwenye ‘My Number One Remix’ huku shangwe likiwa kubwa kwa mashabiki waliojazana hapo.

Baada ya kumaliza show hiyo ya kama dakika 8 hivi, Diamond alisikika akisema kuwa “Nimekuja kumpasupport rafiki yangu tukutane Wasafi Festival,” amesema.

Baada ya maneno hayo alitoka jukwaani na kuondoka akiwaacha watu wakipiga shangwe kubwa sana.
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )