Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Saturday, June 30, 2018

Diwani Chadema anayedaiwa kumbaka mwanafunzi aendelea kusota rumande

Diwani wa Kata ya Kia (Chadema), Yohana Laizer ameendelea kusota rumande baada ya hakimu anayesilikiza kesi yake kutokuwepo mahakamani, ikielezwa kuwa yupo likizo.

Diwani huyo anatuhumiwa kwa makosa mawili ya kumbaka na kumpatia ujauzito mwanafunzi wa shule ya msingi Obrieni iliyopo Kata ya Kia Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro.

Jana Juni 29, 2018 kesi hiyo namba 152 ya 2018 ilipangwa kusikilizwa katika mahakama ya Wilaya ya Hai, lakini imeahirishwa kwa mara ya tatu kutokana na hakimu kutokuwepo mahakamani.

Hakimu wa Mahakama ya Mwanzo Wilaya ya Hai,  Regina Mushi  ambaye kesi hiyo kwa mara ya kwanza ilitajwa mbele yake, alisema  hakimu mwenye mamlaka ya kusikilia kesi hiyo  yupo likizo,  kwamba yeye hana mamlaka ya kuisikiliza kesi hiyo mpaka pale hakimu huyo atakaporejea.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Julai 5, 2018 kwa ajili ya  usikilizwaji wa awali.
Advertisement
Loading...
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
==

taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )

Loading...