Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Saturday, June 30, 2018

Dogo Janja Aponda Mavazi Ya Rayvanny

Msanii wa muziki wa Bongo fleva anayefanya vizuri na ngoma yake ya ‘Banana’ Dogo Janja amedai msanii kutoka label ya WCB Rayvanny anamuangusha sana Kwenye suala la mavazi.

Siku za nyuma Dogo Janja ameshawahi kuachia ngoma maalumu kwa ajili kuvaa na kupendeza Inayoitwa ‘Ukivaaje unapendeza”.

Kwenye mahojiano na Wasafi Tv, Dogo Janja amefunguka na kuweka wazi kama  akipata fursa ya kumvalisha Rayvanny atafanya hivyo.

"Nikiambiwa msanii ambaye niwe namvalisha namchagulia mavazi, nitamchagua Rayvanny huwa ananiangusha sana sometimes.

"Kuna muda huwa anapatia halafu kuna muda unaweza ukatema mate kule, anaweza akala njano juu mpaka chini”.

Dogo Janja yupo katika Media Tour kwa ajili ya kutangaza rasmi Single yake mpya ‘Banana’ inayoendelea kufanya vizuri Kwenye chati mbali mbali.
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Loading...
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )