Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Saturday, June 23, 2018

Inasemekana Infinix Kushirikiana Na Google Katika Uzinduzi Wa Simu Mpya Barani Afrika.

inasemekana kampuni ya simu ya Infinix kuzindua simu mpya ikiwa ni muendelezo wa Infinix NOTE 4 kwa kushirikiana na GOOGLE. Uzinduzi huo unategemewa kufanyika mnamo mwezi wa sita barani Afrika nchini Dubai katika jengo la Burj Khalifa.
 
Kwa pamoja ikishirikiana na GOOGLE kampuni ya simu ya Infinix imeweka nia ya kuzindua simu iliyo na ubora zaidi ya matarajio ya wengi na inasemekana kupitia ushirika wake na GOOGLE ujio wa simu zote za NOTE kutumia mfumo wa Android 1 (A1) wenye ufanisi zaidi ya Android Oreo.
 
Zaidi ya watu 200 mpaka sasa wameshapata mwaliko kutoka katika kampuni hizo mbili kwenda kushuhudia uzinduzi huo pamoja na kushuhudia namna Android 1 (A1) inavyofanya kazi kupitia GOOGLE Assistant na GOOGLE Lens.
 
 Akiongelea mafanikio ya kampuni, muongeaji wa kampuni ya Infinix Bwana Erick Mkomoye alisema kwamba, “tangu kutambulishwa kwa kampuni ya Infinix mwaka 2013, kampuni imeweza kudhihirisha ubora wake na kuweza kupenya katika masoko ya Afrika na tuko mbioni kuwaletea teknolojia mpya kupitia simu mpya itakayozinduliwa wiki ijayo.
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Loading...
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )