Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Wednesday, June 20, 2018

Irene Uwoya Awatolea Uvivu Wanaomponda Kwa Mavazi Aliyovaa

adv1
Msanii wa filamu nchini Irene Uwoya na mke halali wa mwanamuziki Dogo Janja amewatolea uvivu mashabiki zake kwenye mtandaoo wa kijamii kuwa sio wa kwanza yeye kuvaa nguo za ufukweni hivyo wasimpangie chakufanya kwa madai vazi hilo mume wake amelipenda nasio vinginevyo.

Uwoya ametoa kauli hiyo asubuhi ya leo kupitia mtandao wake wa kijamii baada ya kupita siku moja tokea alipo-post picha aliyokuwa amevalia vazi jeupe lililokuwa linaonesha maumbile yake ya mwili na kusababisha mashabiki zake kumtolea maneno makali kuwa haheshimu ndoa yake wala mume wake kwa kuwa anachokifanya sasa hakipendezi na wadhfa wake aliokuwa nao.

"Ukivaa nguo kawaida ana kigodoro, nikim-post mume oonh mdogo na nisipo post kwanini hum-post mara humpendi. Nikivaa nguo za ufukweni nipo uchi mke wa mtu, sasa nasema hivi kwa wale iliyowauma poleni sana siku nyingine ntawashirikisha nikitaka ku-post. Hivi kwani mimi ni wa kwanza bongo kuvaa hivi maeneo ya ufukweni. Mume wangu kaipenda balaah yani", ameandika Uwoya.

Kwa tamaduni za kiafrika na kitanzania mara zote watu wanaamini endapo mwanamke atakapokuwa ameolewa basi kuna mavazi huwa anaepuka kuyavaa hata kama akiwa kwenye fukwe za bahari na hicho ndicho mashabiki zake walichokiamini lakini kwa bahati mbaya leo wamekutana na jambo la utofauti.
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )