Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Wednesday, June 20, 2018

Jeshi La Polisi Shinyanga Linachunguza Mauwaji Ya Wanaume Wawili.

Na, magdalena kashindye
Jeshi la polisi mkoani shinyanga linafanya uchunguzi wa vifo vya kutatanisha vya wanaume wawili vilivyotokea Ngogwa wilayani kahama mkoani humo.

Taarifa ya Jeshi hilo kwa vyombo vya habari iliyotolewa juni 20 /2018 na kamanda wa polisi mkoa wa shinyanga ACP Saimon H. Haule  miili ya wanaume wawili ambao hawajafahamika majina yao, kabila na mkazi wanaokadiliwa kuwa na umri wa miaka 25_30 ilikutwa katika eneo la soko la Ngogwa wilayani kahama juni 19 /2018 saa 3:00 asubuhi .

Haule alisema mwili wa mwanaume mmoja ulikutwa na jeraha kichwani linaloashiria alikatwa na kitu chenye ncha kali huku mtu wapili akiwa hana jeraha wala mchubuko.

"Tunaendelea kufanya uchunguzi wa vifo vya wanaume wawili vyenye utata   vilivyo bainika juni 19/2018 huko Ngogwa kahama ili kibaini chanzo cha vifo hivyo "alisema Haule.

ACP Haule alisema miili ya marehemu imehifadhiwa katika  chumba cha kuhifadhia maiti  hospital ya halmashauri ya mji wa kahama kwa utambuzi na ametoa wito kwa wananchi kushirikiana na Jeshi hilo kuwabaini waharifa wa tukio hilo.
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Loading...
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )