Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Tuesday, June 26, 2018

Kazi Sasa Imeanza: Ureno Kuvaana na Uruguay Huku Hispania Akikipiga na Urusi

Baada ya mechi nne za jana za kufunga makundi ya A na B kwenye Fainali za Kombe la Dunia kumalizika, hatimaye mechi mbili za raundi ya 16 bora zimefahamika ambapo Ureno itacheza na Uruguay huku wenyeji Urusi wakikabiliana na Hispania

Katika mechi mbili za Kundi B zilizomalizika  jana usiku, zilishuhudiwa zikimalizika kwa sare ambapo Hispania ilitoka sare ya 2-2 na Morocco huku Ureno ikitoka sare ya 1-1 na Iran. Hispania itacheza na mshindi wa pili wa Kundi A ambaye ni mwenyeji Urusi na Ureno itacheza na mshindi wa kwanza Uruguay.

Katika mechi ya Ureno dhidi ya Iran zilishuhudiwa penati mbili ambapo Cristiano Ronaldo alikosa huku Karim Ansarifard akipata kwa upande wa Iran. 

Penati hizo zimefanya michuano hii kufikisha penati 20 hadi sasa ambayo ni idadi kubwa zaidi kuwahi kutokea katika historia ya Fainali za Kombe la Dunia.

Ureno pia wamefanikiwa kusonga mbele kutoka hatua ya makundi kwa mara ya nne katika historia yao ya kucheza Kombe la Dunia. Wamefanya hivyo katika miaka ya 1966, 2006, 2010 na 2018.

Naye mshambuliaji wa Hispania Iago Aspas ambaye alifunga bao la kusawazisha la Hispania, sasa amehusika katika mabao 8 kwenye mechi 8 za Hispania hivi karibuni. Amefunga matano na kusaidia matatu. Hispania pia wamefanikiwa kumaliza hatua ya makundi bila kupoteza mechi tangu wafanye hivyo mwaka 2006.
Advertisement
Loading...
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
==

taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )

Loading...