Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Thursday, June 14, 2018

Kombe La Dunia Kuanza Leo, Wenyeji (Urusi) Wanafungua Michuano Na Saudi Arabia

adv1
Sherehe ya ufunguzi inabidi kuanza nusu saa kabla ya Urusi kucheza mechi ya ufunguzi dhidi ya Saudi Arabia (mishale ya saa 18:00 za jioni) Sherehe hizo zitadumu kwa muda wa nusu saa tu ili kupisha mechi.

Urusi ndiyo wenyeji wa michuano hiyo na wanapewa nafasi kubwa ya kufanya vizuri ingawa timu yao haina wachezaji wenye majina makubwa, mechi hiyo ambayo itaanza saa 12 jioni kwenye Dimba la Luzhinki, inatarajiwa kuonyesha picha halisi ya michuano hiyo itakavyokuwa.

Hofu kwa mashabiki wa Urusi ni kitendo cha nchi yao hiyo kushindwa kushinda mchezo hata mmoja wa kujiandaa na michuano hiyo ingawa wachambuzi wengi wa soka wanaamini kuwa siyo kipimo sahihi.

Timu hiyo iliyopo chini ya kocha Stanislav Cherchesov, ipo Kundi A na Misri, Saudia Arabia wenyewe na Uruguay ambao wanapewa nafasi kubwa ya kuwika kwenye kundi hilo.
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )