Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Saturday, June 9, 2018

Maalim Seif aanza ziara Ya Siku Mbili Pemba

Katibu Mkuu wa CUF Maalim Seif Sharif Hamad ameanza ziara ya siku mbili kisiwani Pemba leo.

Mkurugenzi wa habari wa chama hicho upande wa Maalim Seif, Salim Abdalla Bimani amesema   leo kuwa ziara hiyo ni ya kawaida kwa kiongozi huyo kila ifikapo mwezi wa Ramadhan.

Amesema ziara hiyo haihusiani na harakati za chama bali ni kuwajulia hali wagonjwa na kuwapa pole wafiwa kama ilivyo kawaida yake.

Katika ziara hiyo ya siku mbili anatarajiwa kutembelea mikoa yote miwili ya kisiwa hicho na kisha kurudi kisiwani Unguja kuendelea na ziara kama hiyo katika maeneo mbali mbali.

Bimani amewataka wananchi wa kisiwani hicho cha Pemba kutoa ushirikiano wao wa kina kwa kiongozi huyo wa chama chao .
tangazo
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )