Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Sunday, June 10, 2018

Makamu wa Rais: Hatukatazi Kuikosea Serikali lakini Tumieni Lugha Nzuri

SERIKALI imesema haikatii kukoselewa na mtu au kikundi chochote isipokuwa inachosisitiza ni matumizi mazuri ya lugha  wakati wa ukosoaji na sio kutumia lugha inachochea chuki na migawanyiko miomngoni mwa wananchi.

Kauli hiyo imetolewa leo na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Hassan Suluhu kwenye ibada ya kuwekwa Wakfu Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania , Dayosisi ya Magharibi Kati –Tabora.

Alisema Serikali haina dini lakini watu wake wana dini zao hivyo itaendelea kushirikiana na viongozi wa dini ili kuhakikisha wananchi wanaendelea kutenda mema kwa ajili umoja wa nchini.

Makamu wa Rais alisema Serikali haitamvumilia mtu yoyote ambaye atataka kuwagawa Watanzania kwa misingi ya ukabili, udini na hata itikadi za kisiasa.

Aliwataka viongozi wa dini nchini kuendelea kuhubiri amani kila wakati na kusema kuwa kwa upande wa Serikali amani na usalama wa wananchi ndicho  kipaumbele chake cha kwanza na hivyo itaendelea kuhakikisha Tanzania inabaki na umoja wake.

Naye Mkuu wa Kanisa la KKKT Askofu Dkt. Fredrick Shoo alisema Kanisa linaunga mkono juhudi za Serikali ya Awamu ya Tano katika za kupigania haki mbalimbali za Watanzania.

Aliitaka Serikali kuwachukulia hatua wale wote ambao wanataka kulichonganisha Kanisa hilo na Serikali kwa tumia mitandao na vyombo mbalimbali kwa ajili ya maslahi yao binafsi.

Askofu Shoo alisema Kanisa litaendelea kutumia njia za kistarabu kuishauri Serikali na kama kukitokea tofauti watajadiliana na kumaliza mambo kistarabu na sio kama watu ambao wana nia mbaya wanavyochochea.

Kwa upande wa Askofu wa Kwanza wa Dayosisi ya Magharibi Kati –Tabora Askofu Dkt. Isaac Kissiri Laiser alisema Kanisa hilo lipo tayari katika kushirikiana na Serikali katika ujenzi wa Viwanda mkoani Tabora ili kuelekea katika uchumi wa kati.

Katika sherehe hizo Makamu wa Rais aliichangtia Dayosisi hiyo milioni 3 kwa ajili ya kuongezea katika azma yao ya kujenga Kituo cha Afya.
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Loading...
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )