Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Tuesday, June 5, 2018

Mbunge Amtaka Spika Arudishe Matangazo LIVE Ya Bunge

adv1
Mbunge wa Viti Maalum (CUF), Riziki Lulida amemwomba Spika wa Bunge, Job Ndugai kurejesha matangazo ya Bunge yaonekane moja kwa moja.

Akichangia bajeti ya Wizara ya Fedha na Mipango ya mwaka 2018/19 jana  bungeni, Lulida alianza kwa kumpongeza Spika Ndugai jinsi alivyounda kamati za Bunge zilizoonyesha tija kwa Taifa.

“Hongera Spika, umeliamsha dude, tunataka Bunge live, wananchi wanataka kusikia, nini unazungumza na kujua wabunge wanasemaje,” alisema Lulida na kuongeza:

“Tukikaa humu ndani, wananchi hawaoni unayoyafanya na ukifanya hivyo itakuwa jambo zuri.”

Lulida ameiomba Wizara ya Fedha na Mipango kuangazia hujuma zinazofanywa katika mashine za kielektroniki (EFDs) kwa kuhakikisha kunakuwapo na mifumo imara ya usimamizi kwani baadhi ya watu wanaweza kuwa na njama za kuihujumu.
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )