Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Monday, June 11, 2018

Mwalimu anayedaiwa kudhalilisha wasichana St. Florence mbaroni

adv1
Jeshi  la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam linamshikilia mwalimu wa Shule ya Msingi St Florence iliyopo Mikocheni, anayedaiwa kudhalilisha kijinsia wanafunzi wanne wa kike wa darasa la saba. 

Taarifa za kudhalilishwa kwa wanafunzi hao, zilianza kusambaa kwenye mitandao ya kijamii, zikieleza kuwa mwalimu huyo amekuwa akiwadhalilisha watoto hao.

Mwalimu huyo, ambaye polisi haikutaja jina lake, inadaiwa alifanya tukio hilo wakati akiwa na wanafunzi hao katika ziara ya kimasomo.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu, Lazaro Mambosasa alisema mwalimu huyo amekamatwa na wanaendelea na upelelezi. Mambosasa alisema hawezi kueleza kwa undani kuhusu kukamatwa kwa mwalimu huyo, kwa kuwa yapo masuala ya kiupelelezi yanaendelea, hivyo anahofia kuharibu upelelezi.

“Siwezi kusema sana kwa undani lakini mtuhumiwa amekamatwa na tunaendelea na upelelezi unatakapokamilika hatua za kisheria zitachukuliwa,” alisema Mambosasa. 

Awali, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Jumanne Muliro alisema polisi ilipata taarifa na iliendelea kumsaka mwalimu huyo tangu Mei 24 mwaka huu. 

Muliro alisema walishafanya mahojiano na wanafunzi wanaodaiwa kufanyiwa udhalilishaji huo na walikuwa wakisubiri kukamatwa kwa mwalimu anayetuhumiwa
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )