Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Friday, June 22, 2018

Mwanamke Auawa Manyara, Chanzo Cha Kifo Bado Hakijafahamika, Mmoja Ashikiliwa Na Polisi

Na. Vero Ignatus , Manyara.
Mwanamke mmoja aliyefahamika kwa jila la Josephine Peter (51)mkazi wa Mrara kata ya Mamire wilayani Babati  ameuawa na watu wasiofahamika  huku shingo yake ikikatwa na kitu chenye ncha kali.

Akizungumza jana june 21 Kamanda wa polisi  mkoani Manyara  Augustino Senga amethibitisha kutokea kwa tukio hilo, amesema mwanamke huyo alifariki dunia juni 19 saa 4 usiku akiwa nyumbani kwake  na mtu mmoja anashikiliwa na jeshi la polisi kwa uchunguzi zaidi kutokana na mauaji hayo.

Kamanda amesema kuwa hadi sasa chanzo cha mauaji hayo hakijafahamika kwani mwili wa marehemu umefanyiwa uchunguzi nakubainika  kuwa hajabakwa kama watu wanavyozusha  bali jeshi la polisi unaendelea na upelelezi wa tukio hilo la mauaji amesema kuwa ukikamilika taarifa kamili itatolewa

Mwili wa marehemu huyo umehifadhiwa kwenye hospitali ya mji wa Babati (Mrara)
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Loading...
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )