Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Wednesday, June 20, 2018

Mwanaume amuua mkewe kwa kumchoma Kisu kisha na yeye mwenyewe kujichoma kisu tumboni na kufariki dunia

Kwamba tarehe 19.06.2018 majira ya saaa 05:00hrs alfajiri katika nyumba ya kulala wageni iitwayo Angel Guest House iliyopo kijiji cha Kanyara kilichopo kata ya Buliyaheke wilaya ya Sengerema mkoa wa Mwanza, mwanamume mmoja aliyefahamika kwa jina la Michael Daud @mwanzamila, miaka 31, mkulima na mkazi wa kijiji cha Bukokwa, anatuhumiwa kumuua mkewe aitwaye Tecla Kamuli @ rutha miaka 30, mkazi wa Bukokwa.

Hii ni baada ya kuzuka ugomvi kati ya wawili hao wakati wakiwa wamelala katika nyumba ya kulala wageni ndipo inasemekana mwanaume aliamka kisha alimchoma mkewe na kitu chenye ncha kali katika sehemu mbalimbali za mwili wake hadi akafariki dunia ndipo baada ya kuona hali hiyo na yeye mwenyewe alijichoma kisu  tumboni na baadae alifariki dunia, kitendo ambacho ni kosa la jinai.

Awali inadaiwa kuwa wanandoa hao walikuwa na ugomvi wa muda mrefu katika familia yao, hali iliyopelekea mwanamke kuondoka nyumbani kwao kijiji cha Bukokwa kisha kwenda kupumzika kwa wakwe zake kijiji cha Kanyara.

Inasemekana kuwa  tarehe 18.06.2018 mwanaume alimfuata mkewe kijijini kwao Kanyara lakini hakufika nyumbani kwa wazazi wake bali alifikia kwenye nyumba ya kulala wageni kisha alimuita mkewe wakakutania hapo, ndipo majira tajwa hapo juu inadaiwa ulizuka ugomvi kati yao uliopelekea mwanaume kumchoma mkewe na kitu chenye ncha kali kisha baadae na yeye aliamua kujichoma kisu tumboni na baadae wote wawili walifariki dunia.

Inadaiwa kuwa wahudumu wa Geust hiyo walisikia kelele za mtu akiomba msaada ndipo walifuatilia  kelele hizo zinapotokea ndipo baadae waliona tukio hilo kisha walitoa taarifa polisi. 

Askari walifanya ufuatiliaji wa haraka hadi eneo la tukio na kukuta marehemu wote wawili wakiwa tayari wamefariki dunia. 

Miili ya marehemu wote wawili tayari imefanyiwa uchunguzi na daktari na kukabidhiwa kwa ndugu wa marehemu kwa ajili ya mazishi.

Kamanda wa polisi mkoa wa mwanza Naibu Kamishina wa Polisi Ahmed Msangi anatoa wito kwa wananchi wa jiji na mkoa wa mwanza hususani wanandoa akiwataka kuacha tabia ya kujichukulia sheria mkononi pindi wanapokuwa kwenye migogoro ya ndoa kwani ni kosa kisheria, bali ni vyema wawaeleze wazee, viongozi wa dini au vyombo vya dola ili wayasuluhishe matatizo yao kisha waendelea kuishi kwa amani.
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Loading...
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )