Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Tuesday, June 19, 2018

Mwenyekiti CHADEMA Ashambuliwa kwa Mapanga na Mishale

adv1
Mwenyekiti wa Kijiji cha Mwikatsi wilayani Babati mkoani Manyara, Simon Lala (CHADEMA) ameshambuliwa na watu wasiojulikana waliomjeruhi kwa mishale na mapanga kwa kile kilichodaiwa kuwa ni mgogoro wa ardhi.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara, Agustino Senga amesema  kuwa shambulio hilo limetokea Juni 18, 2018 katika kitongoji cha Waloa wakati mwenyekiti huyo kwa tiketi ya CHADEMA akiwa kazini pamoja na wajumbe wa serikali ya kijiji.

Kamanda Senga amesema kuwa mwenyekiti huyo ameshambuliwa akitekeleza majukumu yake ambapo alikuwa akisimamia kesi ya ndugu wakigombea ardhi na ndipo upande wa walioshindwa hawakuridhishwa na matokeo ya baraza la kata.

“Tukio lilitokea mida ya saa 5:00 asubuhi wakati mwenyekiti akiwa shambani akimuonesha mipaka ndugu wa watuhumiwa hao waliokimbia baada ya kutekeleza shambulio hilo, ambao walishindwa katika kesi ya kugombea ardhi lakini hawakuridhishwa na matokeo na kudai mwenyekiti kafanya upendeleo”, amesema Kamanda.

Kwa upande wake Katibu wa CHADEMA Mkoa wa Kilimanjaro, Basil Lema amesema mwenyekiti huyo atahamishiwa katika Hospitali ya Rufaa ya KCMC kwa matibabu zaidi baada ya kupewa rufaa katika Hospital ya Mkoa wa Manyara.

adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )