Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Thursday, June 21, 2018

Mwijaku Amchana Uwoya: “Irene Hana Marafiki Wa Kweli, Shamsa Ford ni Mnafiki”

Muigizaji wa Bongo movie maarufu kama Mwijaku amemmwagia povu zito msanii mwenzake Irene Uwoya baada ya picha yake kusambaa siku ya jana.

Siku ya jana Irene aliposti picha iliyozua utata Kwenye mitandao ya kijamii na mara moja Mwijaku alimwandikia posti nzito ambayo alimsema sana kwa vazi lile hasa kwa sababu ni mke wa mtu.

Lakini Mwijaku hakuishia hapo kwani Kwenye mahojiano aliyofanya na Millard Ayo Tv, Mwijaku alionekana akiweka wazi Kuwa marafiki zake na a Uwoya wanaomsapoti kwa picha zile ni wanafiki wakubwa kwani wanamshauri vibaya wakijua wazi kabisa picha ile siyo nzuri:

"Irene ni mtu mzima na mke wa mtu na hii ni ndoa yake ya pili kwa nini aposti picha kama ile? Nikajiuliza Marehemu Ndikumana angekuwepo wakati amemuoa angeweza kuposti kitu kama kile? Asingeweza kuposti Ndikumana alikuwa mkali ila kwa sababu mume wake Dogo Janja ni mdogo basi anamuonea.

"Halafu na marafiki wanaomzunguka Irene ni wanafiki siku akija kufa atakuwa peke yake halafu na Shamsa Ford anaenda kumwambia hivyo hivyo umependeza ishi utakavyo! Tuongee ukweli Shamsa Ford ni mnafki na anampoteza mwenzake”.

Dogo Janja ambaye ni mume wa Irene Uwoya aliweka wazi kuwa hakukerwa na picha ile zaidi alimpa sapoti mke wake....Tazama Alichoandika

Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Loading...
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )