Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Monday, June 25, 2018

Padri anayetumia muziki wa Hip Hop kanisani kushawishi vijana kuhudhuria ibada asimamishwa kazi

 Padri wa Kanisa Katoliki nchini Kenya aliyepata umaarufu kutokana na mtindo wake wa kutumbuiza kwa kutumia muziki wa kufoka amesimamishwa.

Paul Ogalo jina maarufu 'Sweet Paul' amekuwa akitumia muziki wa rap kama njia ya kuwavutia vijana wengi kufika kanisani.

Alikuwa akisema muziki ni njia sahihi si tu kuwavutia vijana bali pia kueneza Injili.

Miongoni mwa nyimbo zake alizokuwa akiimba ni pamoja na "Kujeni church kuna baraka, kujeni church kuna baraka..." au "Father Paul, niki-lock kwenye mic, Nduru (fedha) inafuata, mamanze go tipsy, vijana ruka ruka swag ya kunguru, au sio"

Lakini hatua yake hiyo inaonekana kutowafurahisha viongozi wa Kanisa Katoliki Magharibi mwa Kenya ambao wamemsimamisha kazi kwa mwaka mmoja ili ajitafakari.

Askofu wa jimbo la Kanisa Katoliki la Homa Bay, Philip Anyolo amesema padri huyo ni lazima achague kati ya kuwa rapa na kuwa padri.

Amesema kasisi huyo hataruhusiwa kuongoza ibada ya misa kwa kipindi cha mwaka mmoja ingawa anaruhusiwa kushiriki ibada, na pia anaruhusiwa kufanya ibada ya misa lakini faraghani.

Mavazi ya kasisi huyo yalikuwa ni tofauti na mapadri wengine yeye alipendelea kuvaa fulana ndefu za rangi nyekundu au nyeusi, suruali isiyobana mwili pamoja na kujifunga kitambaa kichwani na kutumbuiza kwa nyimbo kama wafanyavyo wanamuziki wa rap.

Hilo limekuwa likiwafurahisha vijana wengi na hata waumini wengine wa umri mkubwa.

Askofu Anyolo amesema uamuzi wa kumsimamisha kazi ulifikiwa mwezi uliopita.

Hata hivyo amesema kasisi huyo yuko huru kuendelea kutumia muziki wa rap na njia nyingine za kutumbuiza kuwahubiria vijana "lakini hafai kufanya hivyo kwenye altari."

"Mambo ya kidini na ya kidunia hayawezi kuchanganywa. Padri Ogallo ana kipindi cha mwaka mmoja cha kujitafakari na kuamua iwapo amejitolea kufuata maisha kamili ya upadri," amesema askofu huyo.

Padri huyo ameliambia Shirika la Habari la BBC kwamba hado hajapata taarifa za kusimamishwa kazi kwake na wakuu wa kanisa, ila amekuwa akisikia tu taarifa mitandaoni.

"Niligundua ya kwamba vijana wanapenda muziki, ndio maana wanaenda maeneo ya burudani, hivyo nikasema kama wanapenda hivyo basi hiyo ndiyo nitawapatia," alisema awali katika mazungumzo yake na BBC.

"Mimi naimba muziki wa aina yoyote, wa injili, riddims, hip-hop, lingala, raga, reggae pamoja, ili niwape mchanganyiko kamili."
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Loading...
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )