Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Thursday, June 21, 2018

Rais Magufuli Atamani Wafanyakazi TTCL Waongezewe Mishahara Kwa Kazi Nzuri Wanayofanya

Kutokana na faida waliyoipata mwaka 2017 hadi kutoa gawio la Sh1.5 bilioni kwa Serikali, Rais John Magufuli amesema wafanyakazi wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) wana haki ya kuongezewa mishahara.

Akizungumza leo Juni 21 wakati wa hafla ya Serikali kupokea gawio hilo kutoka TTCL, Rais amesema hata kama hajapandisha mishahara kwa watumishi wote wa Serikali lakini shirika hilo limeonyesha jinsi linavyotanguliza masilahi ya Taifa mbele.

“Tangu shirika hili lianzishwe mwaka 1993 halijawahi kutoa gawio. Uchapakazi wenu unaonekana. Ingawa sijaongeza mishahara kwa watumishi lakini ninyi ayayaya,” amesema Magufuli.

Serikali imepokea gawio kutoka shirika hilo ukiwa ni mwaka mmoja tangu lilipobadilishwa kutoka kuwa kampuni na kuanza kujiendesha kwa faida.

Rais ameyataka mashirika ya umma kujiendesha kwa faida na kutoa gawio huku akiyasisitiza kujiendesha kwa ufanisi.

Amesema mwaka 2005 kulikuwa na mashirika 92, lakini ni manne yaliyotoa gawio la Sh130.868 bilioni.

Baadaye yaliongezeka mashirika 24 yaliyotoa gawio la Sh149.3 bilioni mwaka 2006 na mwaka 2007 mashirika 38 yaliipa Serikali Sh677 bilioni.
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Loading...
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )