Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Friday, June 15, 2018

Rais Magufuli Atoa Zawadi Za Idd kwa Watu Wenye Mahitaji Maalum

adv1
Habari na Wizara ya Afya.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ametoa zawadi ya Idd El Fitri zenye thamani ya shilingi 11,370, 000 kwa vituo 5 vya Mkoa wa Dar es Salaam, vituo 2 vya Zanzibar na vituo 17 kutoka mikoa ya Tanzania Bara.

Zawadi hizo zimekabidhiwa leo katika Mahabusu ya Watoto iliyoko Upanga Jijini Dar es Salaam na Kamishina Msaidizi wa Ustawi wa Jamii, Idara ya Ustawi wa Jamii, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee, na Watoto, Bw. Rabikila Mushi kwa niaba ya Mhe. Rais, Dkt. John Pombe Magufuli.

Bw. Mushi amezitaja zawadi zilizotolewa kuwa ni mchele, mbuzi na mafuta ya kupikia ambazo zitawezesha makundi hayo kufurahi na kusherehekea sikukuu kama ilivyo kwa watu wengi.

“Mhe. Rais kwa upendo wake wa dhati kabisa ameona umuhimu wa kushiriki pamoja na watu walio katika makundi maalum wakiwemo watoto walio katika mazingira hatarishi na wazee  wenye ulemavu wasiojiweza, wanaohudumiwa  katika makazi, katika kusherehekea sikukuu ya Idd El Fitri mwaka 2018,” amesema Bw. Mushi.

Aidha, amevitaja vituo vilivyonufaika na zawadi za Mhe. Rais kwa Mkoa wa Dar es Salaam ni Dar Al Arquam, Makao ya Taifa ya watoto Kurasini, Makao ya Watoto yatima kurasini,Makao ya watoto yatima  Mburahati, Makao ya wazee wasiojiweza Nunge Temeke na Mahabusu ya watoto ya Taifa Upanga.

Vile vile, amevitaja vituo vilivyonufaika kwa upande wa mikoa ya Tanzania Bara kuwa ni Vituo vya Watoto yatima vya Renato Granti na Bulongwa vyote vya Njombe, Makazi ya Wazee wasiojiweza Magugu mkani Manyara, Makazi ya Wazee ya Taifa  wasiojiweza Fungafunga Morogoro, na baadhi ya vituo vingine vya binafsi na Taifa Nchini.

Kwa upande wa Zanzibar, vituo vilivyonufaika ni Kituo cha Watoto Mazizini cha Mjini Unguja na Makao ya Wazee Limbani Pemba.

Utoaji zawadi hizi umekuwa wa kawaida kwa Wahe. Marais wa Tanzania kwa awamu zote nne kutoa zawadi  za vyakula kama vile mafuta, mchele na mbuzi ili kuwawezesha kufurahi na kusherekea Siku kuu kama ilivyo kwa watu wengine.
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )