Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Thursday, June 21, 2018

Rais Magufuli Awataka TTCL Wasibweteke

Rais John Magufuli amelitaka Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) kutobweteka baada ya kupata mafanikio makubwa.

Amesema kama TTCL itajiona imefanikiwa na kuendelea kubweteka, itajikuta ikitoka katika reli na kupoteza mafanikio yake.

Rais Magufuli ametoa kauli hiyo leo Juni 21 wakati akipokea gawio la Sh1.5 bilioni kutoka shirika hilo.

 “Nawapongezeni sana kwa mafanikio haya mliyopata katika kipindi cha miaka miwili, hongereni sana. Lakini hata hivyo itakuwa ni jambo la aibu sana kama mafanikio mliyopata yakawafia mikononi,” amesema.

Rais amesema pamoja na mafanikio hayo pia waangalie namna ya kuendelea kuboresha huduma na kuangalia njia nyingine za kujiongezea kipato.

“Pia angalieni uwezekano wa kupunguza gharama ili muendelee kupata wateja zaidi,” amesema.
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Loading...
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )