Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Friday, June 29, 2018

Rais Magufuli kufanya ziara ya kihistoria nchini Kenya

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli anatarajiwa kuzuru nchini Kenya mwezi ujao katika ziara ambayo itakuwa ya kihistoria.

Rais Magufuli kwenye ziara yake ataungana na Rais Uhuru Kenyatta na kiongozi wa upinzani nchini humo Raila Odinga na kisha kutembelea katika Kaunti ya Nyanza.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na gazeti la Nation la nchini Kenya limeeleza kuwa Rais Magufuli anatarajiwa kuwasili nchini Kenya Ijumaa ya wiki lijalo.

Gazeti hilo pia halijaeleza ziara hiyo itakuwa ya siku ngapi na itakuwa na lengo gani katika kipindi hiki ambacho Rais Uhuru Kenyatta na Odinga wameonekana kupatana na kuweka tofauti zao za kisiasa kando.

Hii ni mara ya pili kwa Rais Magufuli kuzuru nchini Kenya ni baada ya kuzuru mwaka jana ambapo alikutana na Rais Uhuru Kenyatta.

Hata hivyo, Rais Magufuli hata kabla ya kukutana na Kenyatta mwaka 2016  kwenye ziara yake nchini Kenya mwaka huo huo alitembelewa na Raila Odinga kijijini kwake Chato..

Ziara hiyo inakuwa ni ya kihistoria na ya kwanza kwa Rais Magufuli kukutana na viongozi hao wawili na wenye nguvu zaidi kwenye siasa za Kenya.
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Loading...
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )