Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Saturday, June 16, 2018

Ronaldo Aanza na Hat-trick Urusi.......Vita Ya Ureno Na Hispania Yamalizika Kwa Mabao 3-3

adv1
Na Magdalena Kashindye.
Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Ureno Christiano Ronaldo ameandika historia ya kuwa mchezaji wa kwanza kupiga hat trick katika kombe la dunia la mwaka 2018.

Katika mchezo huu uliopigwa jana usiku majira ya saa tatu Kati ya ureno na Hispania ilichukua dakika nne tu za mchezo kwa Ronaldo kuanza safari yake ya kupiga hat trick     pale alipoipatia timu yake goli la kuongoza kwa njia ya penati kabla ya Diego Costa kusawazisha dakika ya 24 ya mchezo kipindi cha kwanza.

Dakika ya 44 Ronaldo aliiandikia timu yake goli la pili hadi mapumziko ureno 2_1 .Hispania dakika ya 55 Costa alisawazisha na dakika mbili badae Nacho aliandika goli la tatu kwa Hispania.

Wakati mchezo ukielekea kumalizika Ronaldo akawainua wareno wenzake dakika ya 87 kwa kufunga goli la tatu na kufanya ubao usomeke ureno 3_3 Hispania.
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )