Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Monday, June 25, 2018

Ruby afunguka kuhusu picha zilizosambaa kwenye mitandao ya Kijamii Zikimuonesha Amekonda

Msanii wa muziki Bongo, Ruby amefunguka kuhusu stori zinazodai kwa sasa mwili wake umepungua (amekonda) ukilinganisha na hapo awali.

Muimbaji huyo anayetamba na ngoma ‘Niwaze’ ameiambia FNL ya EATV kuwa picha zilizokuwa zikisambaa kwenye mitandao hajui zimetokea wapi.

Ruby alienda mbali zaidi kwa kueleza kuwa picha hizo zimefanyiwa editing na wale wanaoeneza stori hilo wampe kazi (show) ili anenepe.

"Ile ni picha nasio Rubby halafu mnasema nimekonda kwani mlishawahi kuniona nimenenepa ?, haingii akilini kama vitu ambavyo vya negative wanavyoongea wakati mimi kazi ninafanya, ninaangalia mbele kwenye kazi zangu. Kazi yangu ndio inaongea lakini sio maneno ya watu. Mnaongelea mimi kuonekana mbavu zangu kwanini hamzungumzii kuonekana nina makalio makubwa.

“Halafu kitu kingine basi wawe wanaleta shows, kazi ili tunenepe, hivyo ndio vitu vya kuongea. Kama mnaona tumekonda, mnataka tunenepe, mnaleta shows, kazi,” amesema Ruby.

Ruby alikuwa kimya kwa kipindi kirefu katika muziki mara baada ya kuzinguana na menejimenti yake ya zamani. Wimbo wa kwanza kutoa kwa mwaka huu ni Niwaze aliowashirikisha kundi la The Mafik.
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Loading...
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )