Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Thursday, June 28, 2018

Senegal Yaaga Mashindano Ya Kombe La Dunia..... Yachapwa 1-0 Na Colombia

Senegal imeaga mashindano ya Kombe la Dunia katika mchezo wa kundi H baada ya kukubali kichapo cha bao 1-0 dhidi ya Colombia.

Bao pekee la mchezo huo limewekwa kimiani na Yerry Mina katika dakika ya 74 kipindi cha pili na kuweza kuwapa mkono wa kwaheri Senegal kwenye michuano hiyo.

Wakati huo Poland nayo imeungana na Senegal licha ya kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Japan.

Baadaye kutakuwa na michezo mingine miwili kutoka kundi G ambapo England itakuwa inacheza dhidi ya Ubelgiji huku Tunisia ikimailisha ratiba kwa kucheza dhidi ya Panama kuanzia saa 3  usiku huu.
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Loading...
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )