Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Friday, June 8, 2018

Serikali Kuwashughulikia Maafisa Utumishi wanaochelewesha malipo ya wastaafu

adv1
Serikali imesema mtumishi wa umma anayestaafu anatakiwa kulipwa mafao yake ndani ya siku 60 kwa mujibu wa sheria na kinyume na hapo waajiri watawajibishwa.

Kauli hiyo ilitolewa leo Ijumaa Juni 9, 2018 na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Utumishi na Utawala Bora), Kapteni mstaafu George Mkuchika wakati akizungumza na waandishi wa habari, kupiga marufuku wastaafu kufuatilia mafao yao kwa kuwa kazi hiyo inapaswa kufanywa na maofisa utumishi.

Amesema kumekuwa mateso na usumbufu kwa wastaafu ambao wanachukua muda mrefu kulipwa mafao yao licha ya kuwa ni haki yao.

Kauli ya Mkuchika imekuja huku kukiwa na idadi kubwa ya watumishi wanaosotea mafao yao na baadhi wakitumia muda mrefu na wengine kufariki dunia bila kupata fedha hizo.

"Utakuta mtu anaishi Bukoba lakini anafuata haki yake Dar es Salaam na kila siku analala na kula hivyo kujikuta akitumia gharama kubwa ambazo ni mateso kwake, tunasema sasa mambo kama hayo hayapaswi kuwepo tena,” amesema Mkuchika

Amewataka maofisa utumishi wote kutimiza wajibu wao wa kuwasaidia wastaafu kupata haki yao vinginevyo Serikali haitasita kuwachukulia hatua kali.

Kuhusu hatua za kufuata ili kupata mafao, amesema zinaanzia kwa waajiriwa wenyewe ambao miezi sita kabla wanatakiwa kuandika barua za kueleza mwezi na tarehe za kustaafu kwao kabla ya mwajiri naye kuitaarifu mifuko.

Amesema hatua ya tatu ni kwa mifuko ya pensheni ambayo nayo inatakiwa kuandaa nyaraka muhimu ambazo zitamwezesha mstaafu kupata haki yake mapema.
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )