Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Sunday, June 17, 2018

TCRA yafafanua Kuhusu Watumiaji wa Facebook, Twitter, Instagram Kutakiwa Kujisajili

adv1
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imesema mtumiaji mmoja mmoja wa mitandao ya Facebook, Instagram na Twitter hatakiwi kujisajili.

Taarifa iliyotolewa Juni 16 na Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, James Kilaba imesema taarifa hizo ni za uongo kwa kuwa mtumiaji mmoja wa mitandao ya kijamii hahitaji kusajiliwa na TCRA.

Taarifa hiyo imesema kanuni zinawataka watumiaji wa mitandao kuwajibika kwa maudhui watakayopakia kwenye mitandao hiyo.

Hata hivyo taarifa hiyo imesema wamiliki wote walio na leseni za utangazaji wanaotumia mitambo iliyosimikiwa ardhini (terrestrial) endapo watapenda kutumia mitandao ya kijamii (facebook, instagram na twitter) kurusha maudhui yao kwa lengo la kujisajili, lazima wajisajili kwanza TCRA.

Kilaba amesema mamlaka hiyo itaendelea kuchukua hatua za kisheria dhidi ya watu wanaoeneza uongo huo.

adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )