Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Friday, June 22, 2018

TECNO Kuzindua TECNO Spark 2 Rasmi.

Baada ya amsha amsha nyingi kuhusiana na ujio wa TECNO spark 2. kampuni ya simu ya TECNO imeitambulisha rasmi TECNO spark 2 kwa mara ya kwanza katika ukumbi wa tips jijini Dar es Salaam.
 
Katika uzinduzi huo muongeaji wa kampuni ya TECNO, Bwana Erick Mkomoye alitoa shukrani zake za dhati kwa kusema, tunayo furaha kujumuika nanyi katika uzinduzi wa simu yetu ya TECNO spark 2. TECNO spark 2 ikiwa ni muendelezo wa toleo la TECNO spark kampuni imefanya mapinduzi makubwa katika simu hii kama vile teknolojia ya face id yenye kufungua simu kupitia paji la uso, 
 
Bwana Mkomoye aliendelea, “lakini pia tumeona huu ni wakati muafaka kuitambulisha TECNO spark 2 kwajili ya wapenzi wa mpira kwani eneo lake la juu limetawaliwa na kioo chenye uwiano 18:9 na ukubwa wa nchi 6.0HD+” 
 
“TECNO spark 2 imeboreshwa kwa kupitia mfumo wa android 8.1 Oreo wenye kuzuiya uishaji wa chaji kwa haraka na kukupata ufanisi wa kasi zaidi katika simu yako” alimaliza.
 
Uzinduzi ulisindikizwa  kwa wageni waalikwa na kujishinda zawadi mbalimbali kupitia kipindi hiki cha kombe la dunia huku TECNO spark ikiwa  simu rasmi kwaajili ya wateja kungalia mechi kupitia  kioo chake kikubwa.
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Loading...
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )