Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Tuesday, June 12, 2018

TECNO Pouvoir 2 Uhakika Wa Chaji Ndani Ya Masaa 96.

Pamoja ya kuwa kampuni inayosifika katika uzalishaji wa simu zinazotunza chaji, kampuni ya simu ya TECNO imeendelea kudhihirisha ubora wake kwa mara nyengine tena kupitia TECNO pouvoir 2 (TECNO LA7) ikiwa ni muendelezo wa ‘TECNO L series’ yenye betri 5000mAh na mtandao wa 4G.
                         
Na pamoja ya kuwa na betri kubwa aina ya Li-Polymer, 5V2A yenye kujaa chaji kwa haraka na kudumu nayo zaidi ya siku tatu lakini bado kampuni ya simu ya TECNO hakusita kuhakikisha TECNO pouvoir 2 inakuwa na muonekano mzuri kwa kupitia umbo lake jembamba la ‘metallic’ lenye kutawaliwa na wigo mpana wa kioo chenye uwiano wa 18:9.

TECNO pouvoir imebeba kamera mbili nyuma ikiwa na megapixel 13 na flashi mbili za LED na mbele ikiwa na megapixel 8 na LED flashi pamoja na mix flashi zenye kupiga picha nzuri na zenye wang’avu kutokana  na aina ya kioo cha TECNO pouvoir 2 kuwa na upana wa nchi 6.0 HD+ (1440*720) 450nit IPS. Mix flashi inafanya kazi kama ilivyo kwa flashi za kawaida isipokua yenyewe inapatikana ndani ya kioo cha simu na inafanya kazi wakati wa kupiga ‘selfie’ tu.

Na ikiwa simu ya kwanza kwa toleo la ‘TECNO L series’ kuwa na kasi ya mtandao wa 4G lakini pia TECNO pouvoir 2 inaufanisi mzuri zaidi kutokana na processor ya MT6739WA 1.3 ghz Quard-core pamoja na Android 8.1 Oreo na HiOS ya 3.3.
                                      
TECNO pouvoir 2 inatumia aina tofauti tofauti za ‘security’ ikiwamo fingerprint inayopatikana nyuma ya simu na face id yenye kunlock simu kupitia paji la uso na ndio simu ya kwanza ya toleo la ‘TECNO L series’ kutumia face id.
 
Simu hii pia imekuja na memory ya ndani ya GB 16 na GB 2 za ram vinavyoiwezesha simu kuhifadhi mafile mengi na kufanya kazi zaidi ya moja kwa wakati mmoja pasipo kuathiri uwezo wa simu lakini pia TECNO pouvoir inaweza kubeba hadi GB 64 memory ya ziada. 
 
TECNO pouvoir 2 inapatikana katika rangi tatu tofauti nyeusi, gold na city blue.






Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Loading...
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )