Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Sunday, June 24, 2018

Tunisia Maumivu Tena....Ni Baada ya Kupewa Kichapo cha Mbwa Koko na Ubelgiji

adv1
Tunisia imepokea msiba mwingine katika michuano ya Kombe la Dunia baada ya kukumbana na kipigo cha mbwa koko cha mabao 5-2 kutoka kwa Ubelgiji.

Katika mchezo huo wa Kundi G uliopigwa Uwanja wa Spartak, Ubelgiji wamejipatia mabao yao kupitia kwa Romelu Lukaku aliyefunga mawili.

Mabao mengine ya Ubelgiji yaliwekwa kimiani na Eden Hazard aliyefunga mawili pia moja likiwa la penati, pamoja na Michy Batshuayi katika dakika ya 90.

Mabao ya Tunisia yaliwekwa kimiani na Dylan Bronn katika dakika ya 18 ya kipindi cha kwanza na Khaziri dakika ya 90+3.

Msimamo wa kundi hilo unaonesha Ubelgiji ipo kileleni ikiwa na alama 6 kisha ikifuatiwa na England yenye 3 huku Panama na Tunisia zikiwa hazijapata alama yoyote.
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )