Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Saturday, June 16, 2018

Ufaransa Yaanza Vizuri Kombe La Dunia Kwa Kuipiga 2-1 Australia

Ufaransa imefanikiwa kuibuka na ushindi wake wa kwanza katika michuano ya Kombe la Dunia mwaka huu nchini Urusi  wa mabao 2-1 dhidi ya Australia.

Mabao ya mchezo huo yametiwa kimiani na Antoine Griezmann katika dakika ya 58 kwa njia ya mkwaju wa penati na la pili likitiwa kimiani na Paul Pogba .

Bao pekee la Australia liliwekwa wavuni na Mile Jedinak mnamo dakika ya 62 kwa mkwaju wa penati.

Mechi hii imekuwa ya kwanza kushuhudiwa penati mbili ndani ya dakika 90 zikipigwa kwa pande zote.
Ushindi huu wa Ufaransa unawapa alama tatu muhimu kwenye kundi C ambapo baadaye Peru na Denmark watakuwa wanacheza pia kutoka kundi hilo.
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Loading...
==

taboola apo chini
....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )