Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Wednesday, June 13, 2018

Wabunge Wagawanyika azimio la kumpongeza Rais Magufuli Lililotolewa na Simbachawene

adv1
Wabunge wamegawanyika wakati wa kujadili azimio la kumpongeza Rais John Magufuli kwa uamuzi wa kuendeleza mji wa Dodoma na kuupa hadhi ya Jiji.

Azimio hilo limewasilishwa na Mbunge wa Kibakwe (CCM) George Simbachawene leo Juni 13 2018, ambaye katika azimio hilo amewaomba wabunge kuitaka Serikali kukamilisha haraka mchakato wa kuuleta bungeni muswada wa sheria ya kuifanya Dodoma kuwa makao makuu.

Wakichangia azimio hilo wabunge wa upinzani walipinga azimio hilo wakiitaka Serikali kuandaa kwanza mazingira ya miundombinu kabla ya kutangaza kuleta muswada huo wa Sheria.

Akichangia azimio hilo, Mbunge wa Liwale (CUF) Zuberi Kuchauka amehoji Serikali nini kinachotangulia kati ya Sheria na vigezo.

"Hatupingi Dodoma kuwa makao makuu ama jiji. Lakini ni kipi kinatangulia kati ya Sheria na vigezo vya kuwa jiji," amesema.

Mbunge wa Temeke (CUF) Abdallah Mtolea amesema kuwa azimio hilo lilipaswa kutanguliwa na maombi ya fedha kwa ajili ya uboreshaji wa mji wa Dodoma.

Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Mariam Ditopile ameunga mkono azimio hilo na kuahidi kuwa wakazi wa Dodoma watampa ushindi mkubwa Rais Magufuli katika uchaguzi mkuu ujao.

Hata hivyo, Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) Suleiman Jafo amesema Serikali imetenga Sh 35 bilioni kwa jiji la Dodoma ili zitumike katika ujenzi wa miundombinu.
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )