Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Thursday, June 28, 2018

Waziri Mkuu asisitiza wanaume kupima VVU

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewataka wananchi hasa wanaume kupima Virusi vya Ukimwi na wale wenye maambukizi waanze dawa mapema.

Waziri Mkuu ameyasema hayo jana Juni 27 wakati wa uzinduzin wa vituo 51 vinavyojitegemea vya kupima hali ya hewa, Wilayani Bahi, Dodoma.

 “Ugonjwa wa Ukimwi ni hatari na hatari zaidi ni pale wananchi tunapotembea tukiwa hatujiju kama tuna VVU ama hatuna, kwa hiyo mipango ya Serikali ni kila mmoja bora ajijue afya yake kwa kwenda kupima,”alisema.

Pia amewataka viongozi mbalimbali watakapoandaa mikutano yenye zaidi ya watu mia moja kuweka vibanda kwa ajili ya kupima kwani huduma huyo haina gharama.

“Nahamasisha wote kuanzia watumishi na wananchi wote kupima afya zao, tunataka ifikapo mwaka 2020 asilimia 90 ya wananchi wawe wanazijua afya zao hasa wanaume,”alisema na kuongeza:

“Na kwa wale wataokutwa na maambukizi waanze kutumia dawa na uzuri sasa hivi hizi dawa zinaanza kutumiwa mara tu baada ya kugundulika umeathirika.”

Majaliwa ameiagiza Wizara ya Maji na Umwagiliaji na Wizara ya Uchukuzi na Mawasiliano kutenga fedha kwa ajili ya ufuatiliaji na usimamizi wa mradi wa vituo vya hali ya hewa ili wananchi wapate taarifa za hali ya hewa katika maeneo mbalimbali nchini.

Pia amewaagiza wataalamu wa sekta mbalimbali kutumia taarifa za hali ya hewa katika kazi zao ikiwemo kutoa taarifa mbalimbali kwa wakulima na kushauri maeneo gani wanaweza kufanya kilimo.
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Loading...
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )