Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Thursday, June 14, 2018

Waziri Ummy Aziagiza Halmashauri Zote Nchini Kuweka Kambi Za Uchangiaji Damu Mara Tatu Kwa Mwaka

adv1
Na.Alex Sonna,Dodoma
Waziri wa Afya na Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu amezitaka halmashauri zote nchini kuweka kambi za uchangiaji damu mara tatu kwa Mwaka ili kuweza kufikia lengo la kukusanya damu kwa asilimia 60 kwa Mwaka.

Amesema hayo jana wakati  wa kuelekea katika Maadhimisho ya Siku ya Uchangia Damu Duniani ambayo yanatarajiwa kufanyika kesho,Asubuhi katika Jiji la Dodoma maeneo ya Nyerere Square na kuwaomba wananchi na wadau mbalimbali kujitokeza kwa wingi katika Zoezi hilo ambalo ni muhimu kwa Taifa.

Amesema Matukio ya Uchangia damu yamekuwa yakiokoa maisha hasa kwa kina Mama pamoja na Watoto kwa hiyo ni wajibu wa kila Halmashauri kuratibu na kusimamaia zoezi hilo kwa utaratibu mzuri kwani hadi sasa Tanzania imefanikiwa kukusanya kiasi cha Asilimia 45 ya mahitaji ya damu.

Hata hivyo amesema kuwa kiwango cha Damu kinachohitajika kukusanya kwa mwaka kwa mujibu wa shirika la Afya Duniani WHO ni asilimia moja ya idadi ya watu ambapo Tanzania inahitaji kukusanya chupa laki tano na arobaini ambayo bado haijafikiwa.

Pia Mhe.Mwalimu, amesema kuwa kwa sasa watajikita katika kukusanya damu za makundi adimu ambayo yamekuwa yakikosekana kwenye benki za damu kama kundi A negative,B negative, 0 negative na AB negative.

Kwa Upande wa Dk Magdalena Lyimo  ambaye ni meneja wa mpango wa damu salama amesema kuwa bado Tanzania haijafikia idadi ya chupa za damu zinazohitajika huku Kaimu mganga mkuu wa mkoa wa Dodoma Dk.Nasoro Mzee  ameeleza kuwa kiasi cha damu kilichopo mkoa wa Dodoma bado ni kidogo hivyo Wadau wanahitajika kuhamasisha jamii ili iwe na utayari wa kuchangia damu bila wasiwasi

Siku ya uchangiaji damu duniani inaadhimishwa kila ifikapo 14 amapo Tanzania inategeea kuwatumia wasanii mbalimbali katika kuhamasisha uchangiai wa damu ili kuokoa maisha ya watanzania.
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )