Leo June 12, 2018 Mkutano wa kihistoria kati ya Rais wa Marekani Donald Trump na Kiongozi wa Korea kaskazini Kim Jong Un umefanyika nchini Singapore.
Rais Donald Trump wa Marekani na kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un wamemaliza mkutano wa pili wakati wa chakula cha mchana katika ukumbi wa mkutano wa Sentosa Jumanne hii ya June 12, 2018.
Awali
viongozi hao wawili walikutana kwa dakika 40 ana kwa ana wakiwa na
wakalimani wao pekee yao. Hapo tena wakakutana pamoja na wajumbe wao kwa
saa moja nyingine.
Mapema
baada ya kukutana kwa mara ya kwanza Trump alisema mkutano wake na Kim
ulikua "mzuri mzuri sana" na kusema watakua na "uhuisnano mzuri kabisa",
alipozungumza kwa ufupi na waandishi habari.
Miongoni mwa maafisa wakuu wanaoshiriki kwenye mikutano hiyo ni waziri wamambo ya nchi za nje Mike Pompeo, mkuu wa utawala wa White House John Kelly na mshauri wa usalama wa Taifa John Bolton upande wa Marekani. Kwa upande wa Korea Kaskazini yupo Kim Yong Chol, mshauri wa juu wa Kim aliyetembelea Washington hivi karibuni na Waziri wa mambo ya nchi za nje.
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi
==>>... << BOFYA HAPA Kui Install>>
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )