Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Thursday, June 14, 2018

Ziara Ya Ujumbe Wa Idara Ya Maadili Na Nidhamu Ya Chama Tawala Cha Frelimo Kutoka Msumbiji Ilipotembelea CCM Arusha.

adv1
Jana tar. 13 Juni, 2018  Kamati ya Siasa ya Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Arusha imekutana na Ujumbe wa Idara ya Maadili & Nidhamu ya Chama Tawala cha FRELIMO Kutoka Nchini Msumbiji. 

Ujumbe huo uliongozwa na  Katibu wa Sekretarieti ya Kamati Kuu na Gavana wa Jimbo la Mkoa wa  Maputo Nchini Msumbiji Mh. Raimundo Maico Diomba Umekutana na Uongozi wa CCM Mkoa wa Arusha mapema jana Ofisi za CCM Mkoa wa Arusha ili kujifunza mambo kadha wa kadha ikiwemo ni jinsi gani CCM inaweza kusimamia na kuongoza Vikao vya ngazi mbalimbali kwa nyakati mbalimbali pindi kiongozi ama mwanachama anapokwenda kinyume na maadili ya Chama.

“Ama kwa hakika tumejifunza mengi na kubadirishana mawazo  jinsi ya kuboresha Vyama vyetu viendelee kufanya vizuri kwa Wananchi wake ikiwemo kusimamia vyema Maadili kwa wanachama na  Viongozi wake

"Nimependa sana Katiba ya chama cha FRELIMO inayomtambua Mkuu wa Mkoa kama  Katibu Msaidizi wa FRELIMO Mkoa husika lakini pia Katiba ya nchi yao inasema baada ya Uchaguzi Mkuu ilani inayotekelezwa ni ya Chama kilichoshinda nafasi ya Urais," Alisema Robert  Kaseko ambaye ni Mjumbe wa Kamati ya Siasa ya Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Arusha  na kuongeza kuwa;" Urafiki wetu  na ndugu zetu  FRELIMO daima  utaendelea Kulindwa  kwa  nguvu zote."

adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )