Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Wednesday, July 11, 2018

ACT-Wazalendo Waitaka Serikali Isitumie Mabavu Kudhibiti Tafiti Zinazofanywa Nchini

 Chama cha ACT Wazalendo kimeitaka Serikali kutotumia mabavu kudhibiti tafiti zinazofanyika nchini badala yake itoke hadharani na kujibu hoja zinazoibuliwa.

Chama hicho kimetoa tamko hilo leo Julai 11 baada ya kuiona barua mitandaoni iliyoandikwa na Tume ya Sayansi na Teknolojia (Costech) ikiitaka Taasisi ya Utafiti ya Twaweza kujieleza kwa nini wasiadhibiwe kwa kufanya utafiti bila kupata kibali chao.

Akizungumza na vyombo vya habari leo Julai 11 jijini Dar es Salaam, Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mawasiliano, Ado Shaibu amesema ni aibu kwa serikali kudhibiti mpaka shughuli za utafiti.

"Kama barua hiyo ni ya kweli, basi ni aibu kubwa kwa Serikali kudhibiti utafiti. Tutasimama imara kulinda na kutetea hadhi ya utafiti ili mradi utafiti huo uwe unakidhi vigezo," amesema Shaibu.

Amesema Serikali isiogope mapambano ya hoja kwa sababu ina watu wengi wanaoweza kuzungumza na kutetea hoja badala ya kutumia mabavu na kutaka kuiadhibu Twaweza kwa kufanya utafiti wa Sauti za Wananchi.

Amefafanua kwamba kwa miaka mingi Twaweza wamekuwa wakifanya tafiti na Costech walikuwepo, lakini kwa sababu utafiti wao wa hivi karibuni umeigusa Serikali, wamejitokeza wakisema hawajafuata taratibu.

"Ninavyofahamu mimi, taasisi yoyote ikitaka kufanya utafiti lazima iwasiliane kwanza na NBS (Ofisi ya Taifa ya Takwimu). Ni jambo la kushangaza kama utafiti hauwezi kufanyika kama haujapata approval ya Costech, suala hili linaibua mjadala," amesema katibu huyo.

Kuhusu uchaguzi mdogo wa Agosti mwaka huu, Shaibu amesema kamati kuu ya ACT Wazalendo imeamua kushiriki kwenye uchaguzi huo kwenye nafasi mbalimbali.

Hata hivyo, amesema wameunda kamati maalumu ya mashauriano itakayoongozwa na Omary Shaibu Shaaban ili kushauriana na vyama vingine juu ya kusimamisha mgombea mmoja kwenye maeneo ya kimkakati.
Advertisement
Loading...
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
==

taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )

Loading...