Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Wednesday, July 4, 2018

Taarifa Kuhusu Taratibu Za Mazishi Ya Aliyekuwa Mbunge Wa Jimbo La Korogwe Vijijini, Marehemu Stephen Hillary Ngonyani

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai ameongoza kikao cha pamoja baina ya uongozi wa Bunge na familia ya aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Korogwe Stephen Ngonyani maarufu kama Profesa Maji Marefu.

Kupitia taarifa iliyotolewa na kitengo cha Habari, Elimu na Mawasiliano Ofisi Ndogo ya Bunge, imesema kuwa ibaada ya kuaga mwili wa marehemu Ngonyani, itafanyika katika viwanja vya Karimjee kuanzia saa 3:00 asubuhi na baada ya hapo mwili utasafirishwa kwenda wilayani Korogwe mkoani Tanga kwaajili ya mazishi.

“Jumatano tarehe 4 Julai, mwili wa marehemu utaagwa kwa heshima zote za Kibunge katika viwanja vya Karimjee vilivyopo jijini Dar es salaam, kuanzia saa 3:00 asubuhi na baadaye safari ya kuelekea jimboni kwake Korogwe kwaajili ya mazishi itaanza”, imesema taarifa.

Mheshimiwa Ngonyani amefariki usiku wa Jumatatu tarehe 2 mwezi Julai, katika hospitali ya taifa ya muhimbili alikokuwa akipatiwa matibabu, na atazikwa siku ya Alhamis ya tarehe 5, jimboni kwake Korogwe katika makaburi ya Kwa-Mndolwa.
Advertisement
Loading...
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
==

taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )

Loading...