Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Wednesday, July 18, 2018

Diamond atoa ofa kuwasafirisha watu 30 Afrika kusini ‘Birthday ya Tiffah’

adv1
Mwezi Agosti ndio mwezi ambao mtoto wa kwanza wa msanii Diamond Platinumz na Zarina Hassan alizaliwa, Tiffah Naseeb 

Kufuatia sherehe hiyo Diamond Platinumz ametangaza ofa ya kuwasafirisha watu 30 mpaka Afrika Kusini kusherekea siku hiyo ya kuzaliwa kwa mwanae ya kutimiza miaka mitatu.

Diamond amesema sherehe hiyo itachukua siku tatu ambayo ni ijumaa, jumamosi na jumapili.

”Kwakuwa sherehe hii ya kutimiza miaka mitatu kwa Binti angu @princess_tiffah itachukua WeekEnd nzima, yani kuanzia Ijumaa/ Jumamosi na Jumapili ….kwenye kuhakikisha watu wangu hao 30 wanasafiri Salama, wanakula na wanalala sehemu nzuri na kuwa comfortable siku zote wakiwa huko” ameandika Diamond Platinumz.

Sherehe hiyo itarushwa mubashara kupitia kituo cha runinga cha Wasafi. Aidha haijafahamishwa bado namna itakayotumiwa kuwapata watu hao 30 watakaosafiri mpaka Afrika Kusini kusherekea siku ya kuzaliwa kwa Tiffah.
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )