Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Tuesday, July 24, 2018

Diamond Awajia Juu Wanaodai kuwa yeye ni Shoga

adv1
Staa wa Muziki wa Bongo fleva Diamond Platnumz amemwaga povu zito na kuwajia juu watu wote wanaomkosoa na kumuita shoga baada ya kuonekana akiwa amevaa kikuku.

Wiki iliyopita Kuna picha zilisambaa Kwenye mitandao ya kijamii zilizomuonyesha Msanii huyo akiwa amevaa Kikuu Kwenye miguu yake, skendo ambayo ilikamata vilivyo hasa kwenye mitandao ya kijamii na kumjengea picha tofauti kwa  mashabiki wake.
 
Baadhi ya mashabiki hao kwenye mitandao hiyo walikasirishwa na kitendo hicho hivyo kummwagia matusi ya nguoni kutokana na kuchukizwa na kitendo hicho. 

Hoja kuu kutoka kwa mashabiki hao ilikuwa kwamba, jambo hilo haliendani na utamaduni wa Kitanzania na kwamba wanaofanya hivyo ni mashoga na lengo lake ni kuharibu vijana wadogo wa Kitanzania.

Baada ya povu hilo la mashabiki, Global Publishers walimsaka Diamond ili kusikia anajiteteaje juu ya skendo hiyo ya ushoga:

"Kwanza sijui kama kile ni kikuku, nilivaa kama ninavyovaa mikufu au cheni. Niliona ni urembo kama urembo mwingine na kwamba haiwezi kuwa ishu kubwa kama ilivyotokea”.

Diamond aliwakemea wanaomuita Shoga na kuwataka waache mara moja kwani yeye mwenyewe anachukizwa na tabia za mashoga:

"Ninawaomba chondechonde waache kunihusisha na jambo hilo baya, ujue nyuma yangu kuna watu wengi mno wanatamani kuwa kama mimi hasa vijana wadogo.

“Sasa wakiona ninahusishwa na jambo ambalo linapigwa vita nchini mwetu, wataacha kunifuatilia kama mtu wanayetamani kuwa kamawao," alisema Diamond na kuongeza: "Lakini unajua imekuwa ni kasumba kwa watu maarufu kuhusishwa na jambo hilo ili kuwajengea picha fulani kwa mashabikia”.
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )