Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Tuesday, July 24, 2018

Faiza Ally Amtolea Povu Zito Sugu.....Acha Dharau, Siwezi kufuata hela ya matumizi ya Mtoto Mlimani City

adv1
Muigizaji wa Bongo movie na mjasiriamali maarufu Faiza Ally amemjia juu mzazi mwenzake ambaye ni Mbunge wa Mbeya Mjini na msanii mkongwe wa Bongo fleva Sugu.

Sugu na Faiza wamezaa mtoto mmoja anayeitwa Sasha lakini wamekuwa kwenye mgogoro wa kifamilia kwa muda mrefu sana ambapo Faiza amekuwa akidai kuwa Sugu anagoma kumlea mtoto.
 
Wawili hao walionekana kumaliza tofauti zao mwezi uliopita baada ya Sugu kutoka jela ambapo Faiza aliandika Kwenye mitandao ya kijamii kuwa yeye na Sugu wamemaliza tofauti zao.

Lakini Faiza amemtolea povu Tena Sugu jana ambapo kupitia ukurasa wake wa Instagram ameandika:

“Natuma barua kwako kwa sababu sehemu pekee ya kukufikishia ujumbe ukaupata ni hapa ni hivi toka tumeachana sasha ana mwaka na miezi 6 mpaka leo hujatafuta namna sahihi ya kumtunza mwanao sasa tafuta njia sahihi na yenye heshima mimi sio wa kufanyia shopping na happy eti nikachukue mlimani 😂😂😂”

“Hiyo ni zarau sana baba kama ulikosa muda ungetuma hela ! Lazima uweke heshima kwa baby mama wako na mwanao! sasa ni hivi siwezi kwenda kuchukua sukari na maziwa mlimani ni DHARAU!!!!!!” 

adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )