Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Friday, July 6, 2018

Gigy Money: Prezzo Kafulia Choka Mbaya

Video vixen na Msanii wa Muzikiwa Bongo fleva Gift Stanford maarufu kama Gigy Money ameweka wazi msanii kutoka Kenya Prezzo hivi sasa amefulia vibaya mno.

Gigy Money alifunguka hayo wakati anaongelea uhusiano kati ya Rafiki yake Amber Lulu na mpenzi wake Prezzo

Kwenye mahojiano na Kipindi cha XXL cha Clouds Fm, Gigy Money ameweka wazi hivi sasa ukimuona Prezzo siyo yule uliyekuwa unamuona kwenye Tv yaani kafulia:

"Yaani Prezzo kakonda kuliko hata unavyomuona Kwenye picha, naona ni stress za kimaisha kwa sababu mimi nimeenda kuperfom juzi juzi Nairobi nimeondoka club nimemuacha Prezzo mpaka asubuhi saa saba za usiku hana direction yoyote.

"Alikuwa ana jina zamani sio sasahivi, hata wanavyomchukulia huko Nairobi sio tunavyomchukulia sisi huku Bongo yaani amefulia choka mbaya hayupo kwenye peak tena hata huku tunamuongelea sababu ya Amber”.

Gigy Money amedai Kenya wasanii wenye majina ni wasanii kama Nyanshinki, Will Paul, Khaligraph na wengine lakini ukimtaja Prezzo watu watakucheka sana.
Advertisement
Loading...
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
==

taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )

Loading...