Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Friday, July 6, 2018

Hatimaye mwili wa Patrick wawasili Dar es salaam

Mwili wa mtoto wa muigizaji wa filamu nchini, Muna love, Patrick Peter, umewasili nchini leo saa 11:45 jioni na kupelekwa hospitali ya Aga Khan kwa ajili ya kuhifadhiwa.

Taarifa zilizotolewa na Baba Mdogo wa Marehemu, Patrick ambaye ndiye Mwenyekiti wa Kamati ya Mazishi amesema kwamba Mwili huo uliondoka Kenya saa 9:40 jioni.

"Ratiba ya mazishi iko vilevile, kesho mwili utakuja nyumbani kwa baba wa mtoto Mwananyamala kwa ajili ya kuagwa na baadae utaagwa viwanja vya Leaders na utazikwa makaburi ya kinondoni. "Tunashukuru mwili umeshawasili, na tayari tumeshaupeleka Aga Khan kwa ajili ya kuhifadhiwa. "amesema Bazo.

Bazo amesema, baada mwili huo kuwasili ratiba zitaendelea kama zilivyopangwa hapo awali.
tangazo
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )