Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Tuesday, July 10, 2018

Hatma ya dhamana ya mfanyabiashara , Peter Zakaria Kujulikana Leo

Hatma ya dhamana ya mfanyabiashara maarufu Kanda ya Ziwa, Peter Zakaria inatarajiwa kujulikana leo wakati Mahakama ya Hakimu Mkazi Musoma itakapotoa uamuzi kuhusu zuio la dhamana yake iliyowasilishwa na upande wa Jamhuri wiki iliyopita.

Mfanyabiashara huyo anayemiliki kampuni ya mabasi ya Zakaria yanayosafiri kati ya mikoa ya Mwanza, Simiyu na Mara alifikishwa mahakamani Julai 5 akikabiliwa na mashtaka mawili ya kujaribu kuua kwa kutumia silaha baada kwa kuwajeruhi kwa risasi Ahmed Segule na Issac Bwire.

Baada ya kusomewa mashtaka hayo mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Rahimu Mushi, wakili wa Jamhuri, Lukelo Samuel aliiomba Mahakama kuzuia dhamana ya mshtakiwa akidai hali za majeruhi wa tukio hilo lililotokea Juni 29 si nzuri na wamelazwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) kwa matibabu.

Mawakili wa utetezi Kassim Gila na Onyango Otieno walipinga ombi hilo wakisema hakuna nyaraka wala uthibitisho uliowasilishwa mahakamani kuthibitisha kuwa hali za majeruhi ni mbaya na wamelazwa hospitalini.

Baada ya kusikiliza hoja za zote mbili, Hakimu Mushi aliahirisha shauri hilo hadi leo Julai 10 ambapo anatarajiiwa kutoa uamuzi wa kuhusu dhamana.
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Loading...
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )