Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Monday, July 2, 2018

Hii ndio sababu ya Dkt. Mengi kuandika kitabu

adv1
Mwenyekiti wa makampuni ya IPP nchini Tanzania, Dkt Reginald Mengi amesema sababu kubwa ya yeye iliyomsukuma mpaka kufikia hatua ya kuandika kitabu kinachoelezea maisha yake kiujumla ni kutokana na mtoto wake Roodney ambaye ameshafariki kumsisitizia kuandika kitabu.

Dkt, Reginald Mengi amebainisha hayo leo Julai 02, 2018 wakati alipokuwa anazungumza mbele ya wageni viongozi wa nchi na wageni waliohudhuria katika hafla ya uzinduzi wa kitabu chake kilichopewa jina la 'I Can, I Must, I Will- The Spirit of Success' iliyofanyikia katika ukumbi wa Serena Hotel Jijini Dar es Salaam.

"Nilikuwa na mtoto Roodney lakini kabla hajaondoka hapa duniani aliniomba sana niandike kitabu ambacho kitacho kuwa kinaelezea maisha yangu na mambo ambayo nimeyafanya kwa  hiyo nimefanya hivyo kama alivyotaka mwanangu na leo namshukuru Mungu nimeweza kutimiza ahadi yangu", amesema Dkt. Mengi.

Pamoja na hayo, Dkt. Mengi ameendelea kwa kusema "ahadi ya pili aliyonipa ni kunitaka niwe naenda kufanya mazoezi kila siku 'gym' lakini huwa nafanya hivyo mara tatu au nne nasio kila siku, ila kuanzia leo nitamiza hilo".

Mbali na hilo, Dkt. Mengi amesema jambo kubwa lililoweza kumsukuma mpaka leo hii kukizundua kitabu chake hicho ni kutokana na yeye kuzaliwa katika maisha ya kimasikini kitu ambalo ametaka wananchi wafahamu hilo ili nao waweze kujua namna ya kutoka huko na kuwa katika maisha mengine.

Kwa upande wake, Rais Dkt. John Magufuli ambaye ndio alikuwa mgeni rasmi wa hafla hiyo ya uzinduzi wa kitabu cha 'I Can, I Must, I Will- The Spirit of Success' amewataka watanzania na wafanyabiashara wote kiujumla kununua kitabu hicho ili kiweze kuwafundisha katika kutokana na hali ya umasikini huku akiwasisitizia zaidi kufanya kazi kwa bidii na kuacha kusikiliza maneno ya watu ambao wanawakatisha tamaa.
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )